Wizara ya Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari 'NDALICHAKO NA WALIMU TZ'.

Wizara ya Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari 'NDALICHAKO NA WALIMU TZ'.

Taarifa hiyo inadai kwamba Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazovaa wakati wa kazi.
Tunapenda kuwafahamisha umma kuwa taarifa hizi si za kweli. Aidha wizara inawataka watu wote wanaoeneza taarifa za kizushi aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.
Aidha Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza ushushi huu.

Comments

Popular posts from this blog

STORY YA KUSISIMUA

FORM FIVE SELECTION 2016 CHECK HERE

CHOMBEZO FUPI INAITWA ««JAMANI ANKO»» ISOME HAPA