MOTO WA VICHAKANI ULIVYO FIKAA HADI BARABARANI
STORI KUBWA Moto wa vichakani ukafika mpaka Barabarani , ona picha na video gari zilivyoteketea .. By Sadam Chande on July 18, 2015 Kama unasafiri kwenye barabara kubwa kama ya Dar- Mbeya , au Dar- Mwanza au barabara yoyote kubwa ya magari njiani kuna vibao vya tahadhari kwamba usiwashe moto.. ule moto athari yake sio kwenye misitu pekeake, noma inaweza kuhamia hata barabarani !! July 17 2015 barabara kuu ya California-Las Vegas Marekani wameshuhudia hili tukio, moto ulikuwa unawaka tu vichakani.. upepo mkali ukausukuma ule moto mpaka barabarani.. kulikuwa na magari ambayo hayakupona kabisa, yameshika moto na kuishia hapohapo japo watu wa Zimamoto walijitahidi kuzima kwa kisasa kabisa kutumia Helicopter lakini sio gari zote zilizopona. Madereva wa magari na watu waliowabeba wakaona hili sasa balaa, ikabidi wayaache magari na kukimbia.. kilichotishia watu sio moto pekeake, kulikuwa na milio ya milipuko mikubwa ambayo ilitokana na matairi ya ga...