Sasa hivi sio wewe kuwafata TANESCO wakuunganishie Umeme, ni wao ndio wanatakiwa kukufata
Awamu ya tano ya Rais Magufuli imeambatana na maamuzi mapya au yaliyoongezewa ubunifu na nguvu kubwa ya ufatiliaji ambapo kwenye wizara ya nishati boss Profesa Muhongo cheo chake kikiwa ni Waziri wa nishati na madini amekuja na hii mpya.
Tulizoea kuona Taasisi za kibishara kama Benki na taasisi nyingine ndio zinafata Watu kuomba wanunue bidhaa zao au kujiunga na benki ila sasa hivi imehamishiwa TANESCO maana siku zote ilikua Wananchi ndio wananyenyekea TANESCO wawaunganishie umeme kwenye nyumba zao, Waziri Muhongo ameagiza na kuanzia sasa TANESCO ndio watakua wanafata watu kuomba kuwaunganishia umeme.
Profesa Muhongo amekuja na hii mpya na ninamnukuu >>> ‘TANESCO wanaagizwa kuanzia sasa wawafate Wananchi hukohuko vijijini wakiwa na Wakusanya fedha na stakabadhi zao Wananchi walipie hukohuko vijijini, labda ndugu zangu hamkua mnajua… kazi moja tunaifanya TANESCO sasa hivi, ukitaka kuendelea na umeneja tunakutathmini kila baada ya miezi mitatu‘
‘Tathmini yetu ina vigezo vitatu tu, kwanza fedha unazozikusanya ndani ya miezi mitatu na makusanyo yatakufanya ubaki kwenye Umeneja lakini kama hayaongezeki au yanapungua kazi yako inakua imekushinda, pili ni Wateja wapya uliowaunganisha ndani ya miezi mitatu hao ndio watakufanya uendelee kuwa Meneja wa Wilaya, Mkoa au kanda‘ – Profesa Muhongo
Jambo la tatu ni >>> ‘Ni ubunifu wako na umakini wako wa kutatua matatizo ya wateja, umeme kukatikakatika, LUKU kukosekana, nguzo kuanguka kama kila mara tunapokea malalamiko kuhusu matatizo kwenye eneo lako na hatusikii umeyatatua hiyo inakufanya usiwe Meneja wa karne ya 21 wa Tanzania ya karne ya 21‘
Mameneja wa TANESCO watakua wanafanyiwa tathmini mara nne kwa mwaka ambapo ni kila baada ya miezi mitatu na watakaoshindwa kufikia malengo watakua wamejiharibia kazi wenyewe.
Comments
Post a Comment