Rais Magufuli kaeleza kwanini hapendi sana kusafiri nje ya nchi
Tunajua Rais Magufuli amekuwepo nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili kuanzia April 6 2016 mpaka April 7 jioni aliporudi Tanzania, kwenye moja ya maongezi yake mbele ya Wananchi wa Rwanda ameongea pia kuhusu kwanini hapendi kusafiri nje ya nchi na toka achaguliwe October 2015, amesafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza April 2016.
‘Nataka niwaeleze ndugu zangu, mimi sipendi sana kusafiri kwasababu ninapenda kubana matumizi… nimealikwa sehemu nyingi nimealikwa Ulaya lakini na sehemu nyingine bado sijaenda, nilipoalikwa na Muheshimiwa Kagame nimekuja na ninataka niwaeleze ndugu zangu wa Rwanda hii ndio safari yangu ya kwanza kutoka nje ya Tanzania‘ – Rais Magufuli.
Comments
Post a Comment