Posts

Showing posts from February 19, 2017

Mambo 15 ya kufahamu kuhusu kuhamia mtandao

Image
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ kwa kushirikiana na watoa huduma za simu nchini wameanzisha huduma ambayo itamuwezesha mtumiaji wa simu kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba, huduma hiyo inatarajiwa kuanza March mosi Mwaka huu. Leo February 23 2017 kupitia clouds 360 ya clouds TV, Kaimu Naibu Mkurugenzi maendeleo ya TEHAMA kutoka TCRA, Mhandisi Nehemia Mwenisongole amefafanua baadhi ya mambo katika zoezi la kuhama mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu. B OFYA HAPA KUSOMA ZAID

Sayari nyingine saba zagunduliwa,ni sawa na Dunia

Image
Wataalam wa masuala ya anga wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani ,wamefanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua. Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani,Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One. Hata hivyo wana sayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo. Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani,amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi "Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta dunia ya pili,na kwamba sasa si jambo la kusema kama ingelikuwa hivi,bali sasa tunasema ni lini,Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja.C