FORM FIVE SELECTION 2016 CHECK HERE

TAARIFA KWA
UMMA
24-JUNI-2016.
OR-TAMISEMI inawatangazia majina
ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo
vya Ufundi kwa mwaka 2016.
Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka
shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 65,720
wakiwemo wasichana 29,457 na
wavulana 36,263 wamechaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo
vya Ufundi. Kati ya wanafunzi
waliochaguliwa 34,064 wakiwemo
wasichana 13,466 na wavulana
20,598 sawa na asilimia 52
watajiunga na masomo ya Sayansi na
Hisabati; na wanafunzi 30,897
wakiwemo wasichana 15,445 na
wavulana 15,452 sawa na asilimia 47
wamechaguliwa kusoma masomo ya
Sanaa na Biashara na wanafunzi 759
wakiwemo wasichana 220 na
wavulana 539 sawa na asilimia 1
wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya
Ufundi.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga
na Kidato cha Tano mwaka 2016
wataanza muhula wa kwanza tarehe
11 Julai, 2016 na hakutakuwa na
mabadiliko yoyote ya shule.
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti
katika shule walizopangwa kwa
wakati. Endapo mwanafunzi
atachelewa kuripoti hadi tarehe 24
ambayo ndiyo siku ya mwisho ya
kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na
mwanafunzi mwingine aliyekosa
nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo
vya Ufundi mwaka 2016 pamoja na
fomu za kujiunga (joining
instructions) inapatikana kwenye
tovuti ya OR-TAMISEMI ya
www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI
Tumia link hii kupata matokeo
Waliochaguliwa kidato cha tano na
vyuo vya ufundi 2016

Kuangalia ingia hapa

Comments

Popular posts from this blog

STORY YA KUSISIMUA

CHOMBEZO FUPI INAITWA ««JAMANI ANKO»» ISOME HAPA