MOTO WA VICHAKANI ULIVYO FIKAA HADI BARABARANI

STORI KUBWA

Moto wa vichakani ukafika mpaka Barabarani, ona picha na video gari zilivyoteketea..

By

Sadam Chande

on

July 18, 2015

Kama unasafiri kwenye barabara kubwa kama ya Dar-Mbeya, au Dar-Mwanza au barabara yoyote kubwa ya magari njiani kuna vibao vya tahadhari kwamba usiwashe moto.. ule moto athari yake sio kwenye misitu pekeake, noma inaweza kuhamia hata barabarani !!

July 17 2015 barabara kuu ya California-Las Vegas Marekani wameshuhudia hili tukio, moto ulikuwa unawaka tu vichakani.. upepo mkali ukausukuma ule moto mpaka barabarani.. kulikuwa na magari ambayo hayakupona kabisa, yameshika moto na kuishia hapohapo japo watu wa Zimamoto walijitahidi kuzima kwa kisasa kabisa kutumia Helicopter lakini sio gari zote zilizopona.

Madereva wa magari na watu waliowabeba wakaona hili sasa balaa, ikabidi wayaache magari na kukimbia.. kilichotishia watu sio moto pekeake, kulikuwa na milio ya milipuko mikubwa ambayo ilitokana na matairi ya gari kupasuka.

Zaidi ya magari 20 yameungua kwa moto, mengine yalitelekezwa na watu waliokimbia.. na kuna wengine ilibidi wageuze kurudi walikotoka ili kujiokoa… hakuna taarifa kama kuna mtu yoyote aliyefariki ila kuna majeruhi ambao ni watu wawili tu.

Hali ilikuwa mbaya kiasi cha kusababisha hata barabara kufungwa… Hiyo story iko na kwenye Video hapa.

← PREVIOUS STORYJanuary Makamba kuhusu Kingunge, Udiwani na Ubunge CCM Arusha kisa Lowassa? Ajali.. Mhalifu ghorofani.. >> StoriKUBWA

NEXT STORY →Banza Stone alivyozikwa Dar es salaam July 18 2015 ! #RIP

Comments

Popular posts from this blog

STORY YA KUSISIMUA

FORM FIVE SELECTION 2016 CHECK HERE

CHOMBEZO FUPI INAITWA ««JAMANI ANKO»» ISOME HAPA