JINSI ALIVYOZIKWA BANZA STONE
STORI KUBWA
Banza Stone alivyozikwa Dar es salaam July 18 2015 ! #RIP
By: sadam chande
Jana tuliipata taarifa ya kushtua, ilikuwa msiba wa Mwanamuziki ambae kwa Tanzania alikuwa Legend kwenye muziki wa Dansi, Ramadhan Masanja aka Banza Stone… Sauti yake iliwahi kusikika kwenye bendi chache ikiwemo hizi mbili kubwa za Tanzania, African Stars‘Twanga Pepeta‘ na TOT Plus iliyokuwa inaongozwa na Marehemu Kapteni John Komba.
Leo watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao Sinza, kwa ajili ya kumuaga na kumsindikiza Banza Stonekwenye safari yake ya mwisho duniani.
Mazishi yamefanyika kwenye Makaburi ya Sinza Dar es Salaam.
Juma Nature, M2theP na Steve Nyererewakiwa msibani
Swebe pamoja na Wasanii wengine wakiwa msibani.
Jose Mara wa FM Academia na watu wengine msibani Sinza.
Njiani kuelekea makaburini
Watu wakiwa wamejipanga barabarani Sinza kwa ajili ya kupokea Jeneza kuelekea Makaburini.
Wakati wa Mazishi.
Ali Choki akiwa msibani, waliwahi kuwa Bendi moja na Banza Stone wakati fulani.
Umati wa watu waliofika kwenye msiba wa Banza, hapa ni makaburi ya Sinza Dar.
RIP Banza Stone, safari yake Duniani itakumbukwa kwa mengi lakini hasahasa ni kazi ya muziki mzuri wenye ujumbe ambao japo leo hatuko nae lakini muziki na ujumbe wake utaishi milele !!
Zaidi ya wiki mbili zilizopita Banza Stone alifanya mahojiano na AyoTV na kuelezea alichokua akiugua, na hii ni baada ya kuzushiwa kwamba amekufa.
Hii ni moja ya kazi nzuri ambazo na yeye alikuwepo ndani, inaitwa ‘MTU PESA’-AFRICAN STARS (Twanga Pepeta)
Comments
Post a Comment