Posts

Uliiona picha ya Diamond Platnumz kutoboa pua?! ukweli ninao hapa

Image
Kwa saa kadhaa zimeenea taarifa za mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kuonekana katoboa pua, hii habari imepewa nguvu kutokana na picha aliyoipost Diamond mwenyewe kwenye Instagram akionekana katoboa pua. Ukweli ukoje? …ukweli ni kwamba Diamond hajatoboa pua kama wengi walivyodhani ambapo Meneja wake aitwae Sallam aliwajibu hivi mashabiki walioanza kuuliza >>> ‘Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo’ Maneno ya Meneja Sallam yanamaanisha kwamba sio kweli Diamond katoboa pua, ni mchezo tu na baada ya hiyo picha ya kutoboa pua Diamond aliweka picha nyingine inayoonekana hapa chini akiwa fresh kabisa watu wasiendelee kupanic. ULIIKOSA SHOW YA DIAMOND ILIYOVUNJA REKODI YA MR NICE MAREKANI? ITAZAME HAPA CHINI

Wizara ya Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari 'NDALICHAKO NA WALIMU TZ'.

Image
Wizara ya Elimu Sayansi,Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari 'NDALICHAKO NA WALIMU TZ'. Taarifa hiyo inadai kwamba Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazovaa wakati wa kazi. Tunapenda kuwafahamisha umma kuwa taarifa hizi si za kweli. Aidha wizara inawataka watu wote wanaoeneza taarifa za kizushi aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza. Aidha Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza ushushi huu.

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 8 2016 kwenye, Udaku, hardnews na michezo:

Magazeti ya Tanzania yalichoandika leo April 8 2016 kwenye, Udaku, hardnews na michezo: KUYAANGALIA BOFYA HAPA

Sasa hivi sio wewe kuwafata TANESCO wakuunganishie Umeme, ni wao ndio wanatakiwa kukufata

Image
Awamu ya tano ya Rais Magufuli imeambatana na maamuzi mapya au yaliyoongezewa ubunifu na nguvu kubwa ya ufatiliaji ambapo kwenye wizara ya nishati boss Profesa Muhongo cheo chake kikiwa ni Waziri wa nishati na madini amekuja na hii mpya. Tulizoea kuona Taasisi za kibishara kama Benki na taasisi nyingine ndio zinafata Watu kuomba wanunue bidhaa zao au kujiunga na benki ila sasa hivi imehamishiwa TANESCO maana siku zote ilikua Wananchi ndio wananyenyekea TANESCO wawaunganishie umeme kwenye nyumba zao, Waziri Muhongo ameagiza na kuanzia sasa TANESCO ndio watakua wanafata watu kuomba kuwaunganishia umeme. Profesa Muhongo amekuja na hii mpya na ninamnukuu >>> ‘TANESCO wanaagizwa kuanzia sasa wawafate Wananchi hukohuko vijijini wakiwa na Wakusanya fedha na stakabadhi zao Wananchi walipie hukohuko vijijini, labda ndugu zangu hamkua mnajua… kazi moja tunaifanya TANESCO sasa hivi, ukitaka kuendelea na umeneja tunakutathmini kila baada ya miezi mitatu‘ ‘Tathmini yetu ina vigezo vitat

Rais Magufuli kaeleza kwanini hapendi sana kusafiri nje ya nchi

Image
Tunajua Rais Magufuli amekuwepo nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili kuanzia April 6 2016 mpaka April 7 jioni aliporudi Tanzania, kwenye moja ya maongezi yake mbele ya Wananchi wa Rwanda ameongea pia kuhusu kwanini hapendi kusafiri nje ya nchi na toka achaguliwe October 2015, amesafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza April 2016. ‘Nataka niwaeleze ndugu zangu, mimi sipendi sana kusafiri kwasababu ninapenda kubana matumizi… nimealikwa sehemu nyingi nimealikwa Ulaya lakini na sehemu nyingine bado sijaenda, nilipoalikwa na Muheshimiwa Kagame nimekuja na ninataka niwaeleze ndugu zangu wa Rwanda hii ndio safari yangu ya kwanza kutoka nje ya Tanzania‘ – Rais Magufuli.

FOREVER COVER(RUBY) BY CHEMICAL

Image
Download cover ya nyimbo ya Ruby(FOREVER) Iliyo imbwa na msanii wa KIKE(HIP-HOP) Anayeitwa CHEMICAL. BOFYA HAPA KUIDOWNLOAD

Aneth David... msomi wa Chuo kikuu Dsm Tanzania aliyeshinda tuzo ya Mwanasayansi Afrika

Image
Tanzania imepata headlines nyingine baada ya kupata mshindi msomi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Aneth David ambaye ameshinda tuzo ya Mwanasayansi mkubwa ajaye duniani akiwa bado ni Mwanafunzi wa sayansi kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam. Tuzo inaitwa Next Einstein Forum Ambassador na imeandaliwa taasisi ya Next Einstein Forum ambao wanaamini kwamba Einstein anaekuja ambaye alikua Mwanasayansi mkubwa wa Marekani atatoka Afrika, Mwanasayansi huyu aliweza kutabiri mambo yaliyokuja kutokea miaka 100 baadae. ‘Next Einstein Forum wanaamini kuna Wanasayansi wanaofanya mambo makubwa na mazuri na yanasaidia jamii zao lakini wamefichika wapo vichakani, kinachojulikana zaidi kutoka Afrika ni vita njaa na magonjwa’ – Aneth Aneth amesema alipeleka maombi ya kushiriki tuzo hii July 2015 na baadae akapata majibu, kulikua na Watanzania kama watano aliowaona walioshiriki kama yeye lakini yeye ndio akatajwa mshindi, kulikua na Wawakilishi 54 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo kila nchi