SOMA HII.....ITAKUTIA MOYO KATIKA MAISHA YAKO

Watu wengi wameshindwa kufanikiwa katika maisha sababu ya vikwazo walivyokutana navyo na kusababisha kushindwa kufanya jambo fulani,hivyo wamejikuta wakianguka na kukata tamaa ,hivyo basi naomba nikutie moyo Leo,

1.Kushindwa kwako jana haimaanishi utashindwa na Leo,inuka jipanguse na songa mbele.

2.Usiiishi Jana yako ila itumie kama njia ya kujifunza ili leo usikosee palepale ulipokosea Jana.

3.Kilichofanyika,kishafanyika hauna Uwezo wa kubadilisha jambo lililofanyika ila una Uwezo wa kubadilisha jambo unalolifanya Leo ili uwe na kesho nzuri.

4.Tambua hauwezi kuwa na kesho nzuri kama unatumia muda wako mwingi kuifikiria Jana yako.Tumia mda wako mwingi kuifikiri Leo maana ndiyo uliyonayo.

5.Kataa msamiati nashindwa au siwezi katika maisha yako,pamoja na vikwazo  vyote bado tambua inawezekana.

6.Kushindwa sio maisha yako ila ni sehemu ndogo tu ya maisha yako,hivyo tambua hapo ulipo unapita tu kuna mazuri yanakuja mbele.

7.Hata usiku wa manane huisha na jua likachomoza,hivyo hata magumu kwako yataisha na utaona mwanga mpya maishani mwako.

8.Yawezekana kuna mafuriko ya shida na matatizo kwako ila tambua hata mvua nayo huwa hainyeshi milele,nayo pia huisha na mwanga mpya huchomoza.

9.Kuamka mzima Siku ya Leo inamaanisha bado uko katika uwanja wa mapambano na una nafasi kubwa ya kushinda,Siku mpya maana yake anza tena.

10.Tambua kesho yako ni njema na inang'aa sana.

Nakutakia siku njema na mafanikio mema,Kumbuka kumtanguliza Mungu maana pekee ndiye anaeweza kukuongoza katika njia ya salama.

USIBAKI HAPO INUKA,JIPANGUSE SONGA MBELE.

Sadam Chande Magali
0715594768
Hakuna muda mwingine zaidi ya huu.

Comments

Popular posts from this blog

STORY YA KUSISIMUA

FORM FIVE SELECTION 2016 CHECK HERE

CHOMBEZO FUPI INAITWA ««JAMANI ANKO»» ISOME HAPA